" SIKUMMALIZA SHEIKH ABOUD JUMBE MWINYI – "Maalim Seif"
Hio ni nukuu ya Maneno ya Maalim SEIF SHARIF HAMAD juu ya maisha ya hayati mzee ABOUD JUMBE MWINYIMwaka 1984, Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, na Makamo wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Aboud Jumbe Mwinyi, alilazimishwa kujiuzulu katika Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma akishutumiwa kutaka kuvunja Muungano. Kitendo hiki kimekuwa kikichukuliwa na Wazanzibari kama udhalilishaji mkubwa kwa nchi na heshima yao, na msimamo wa serikali tatu, ambao Jumbe anasemekana kuutetea umekuwa ndio msimamo wa Wazanzibari. Kujiuzulu kwa Jumbe kunaunganishwa na tafauti za kimtazamo baina yake na Katibu Mkuu wa sasa wa ACT WAZALENDO Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye hata hivyo anasisitiza katika makala hii kwamba hajawahi kutafautiana na Jumbe kuhusu mtazamo wa Muungano.
Kwanza niweke kumbukumbu sawa. Mwaka 1984 wakati Mzee Aboud Jumbe anajiuzulu nyadhifa zake zote, mimi ni kweli nilikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mkuu wa Idara ya Uchumi na Mipango ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa [NEC] ya CCM, na hivyo kuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi. Hata hivyo wakati huo sikuwa miongoni mwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi. Kwani nilikuwa Waziri wa Elimu wa Zanzibar kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1980. Nikateuliwa kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar na Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeteuliwa kuwa Rais wa Muda wa Zanzibar mara baada ya Mzee Aboud Jumbe kujiuzulu mwaka 1984. Hivyo kuanzia mwishoni mwa 1980 hadi mwanzoni mwa 1984 sikuwa kiongozi katika Serikali ya Mapinduzi.
Pili, tangu Chama cha Wananchi CUF kiasisiwe hapo 1992, sera yake rasmi ni kuwepo kwa Muungano wa serikali tatu: yaani Serikali ya Muungano, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika.
Pengine itakumbukwa kuwa hata Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuwa Chama cha Siasa chochote kile kina haki ya kuwa na sera yake juu ya Muungano. Akasema kuwa kama vile ni haki ya CCM kuwa na sera ya serikali mbili kuelekea serikali moja, CUF wanayo haki hiyo hiyo ya kuwa na sera ya serikali tatu katika Muungano. Mwalimu Nyerere akamalizia kwa kusema kuwa na sera juu Muungano inayotafautiana
Hivyo basi msimamo wangu tangu kuasisiwa kwa Chama cha Wananchi, CUF haujapata kubadilika. Ni msimamo na sera ya Chama changu cha CUF. Sera ya kuwepo kwa serikali tatu katika Muungano wetu.
Hivyo niseme, kama nilivyokuwa nikisema kila nilipopata nafasi, kuwa bila ya kuubadili muundo wa Muungano wetu kutoka muundo wa sasa wa serikali mbili kwenda kwenye muundo wa serikali tatu, matatizo ya Muungano yataendelea kuutafuna Muungano wetu. Badala ya kuuimarisha tutakuwa tunaendelea kuudhoofisha. Kuimarisha Muungano sio kuongeza orodha ya Mambo ya Muungano katika Katiba. Hili linadhoofisha Muungano. Kwani nguvu za Muungano zitatokana na wananchi wa pande mbili kuukubali kwa dhati Muungano wenyewe. Kuhakikisha kuwa wananchi wa pande zote mbili wanaridhika na muundo wake, mamlaka na madaraka ya kila upande na serikali yake. Na zaidi kuliko yote, wananchi wa pande zote mbili kuridhika kuwa wanatendewa haki katika Muungano.
Vyenginevyo tutakuwa tukibadili misamiati tu: mara tutayaita matatizo ya Muungano; mara tuziite kero za Muungano, pengine tutakuja kuyaita mapungufu ya Muungano, au hata bughdha za Muungano, na kadhalika.
Suala la kutoka serikali mbili kwenda serikali moja hilo halitakubalika.
Baada ya kuweka msimamo huo, sasa nigeukie mambo mengine uliyoniuliza.
Kwamba Mzee Aboud Jumbe alituhumiwa kutaka kuwepo kwa muundo wa Muungano wa serikali tatu na akalazimishwa kujiuzulu. Wakati huo mimi nilitetea muundo wa sasa wa serikali mbili.
Ili hili lifahamike vyema na wananchi ni vyema kwanza kuelezea mazingira yaliyomfikisha Mzee Aboud Jumbe kujiuzulu.
Nitangulie kueleza kuwa mimi binafsi na kwa dhati ya nafsi yangu namuheshimu na namthamini sana Mzee Aboud Jumbe. Kwanza ni mwalimu wangu nilipokuwa nasoma katika skuli ambayo wakati huo ikiitwa The King George VI Secondary School (sasa Lumumba College).
Pili, ni Mzee Aboud Jumbe ambaye alisababisha mimi kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya yeye kuwa Rais wa Zanzibar mwaka 1972, baada ya kukaa kwa miaka minane (8) tangu nilipomaliza masomo ya Kidatu cha Sita (Form VI) hapo 1963 na kuzuiwa na Serikali ya Mapinduzi kujiunga na masomo ya Chuo Kikuu, pamoja na kuwa kila mwaka nilikuwa napata nafasi katika vyuo mbali mbali duniani.
Tatu ni Mzee Aboud Jumbe huyo huyo aliyesababisha mimi kuwa kiongozi katika Serikali ya Mapinduzi na kuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa CCM. Hivyo namshukuru na katu siwezi kumsahau kwa mchango wake mkubwa ulionifanya nilivyo.
Sasa nirejee kuelezea mazingira ya wakati huo ambayo yalikuwa kama ifuatavyo:
Nianzie mwaka 1982 ambapo kulikuwa na uchaguzi wa viongozi wa CCM. Katika kipindi kilichotangulia
Kwa lugha ya sasa unaweza ukaliita kundi la Wahafidhina. Kundi la Frontliners lilikuwa na vijana, damu mpya iliyoingia katika uongozi wa Chama na SMZ. Kundi hili lilitaka mabadiliko katika uendeshaji wa mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Unaweza ukaliita kundi la Reformers.
Uchaguzi wa viongozi wa kitaifa (Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa) wa 1982 ulishuhudia msuguano mkali kati ya makundi hayo mawili. Nia ya Liberators ilikuwa ni kuhakikisha kuwa Frontliners hawaingii katika Halmashauri Kuu ya Taifa. Nia ya Frontliners ilikuwa ni kuhakikisha damu mpya inaingia katika kikao hicho kikuu cha maamuzi cha Chama ambacho wakati huo kilikuwa ndio kimeshika hatamu zote za uongozi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bahati njema Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, kwa busara zake, uliwaingiza watu kutoka makundi yote mawili katika NEC na, baadaye, NEC ikawaingiza watu kutoka makundi yote mawili katika Kamati Kuu.. Frontliners walishukuru kuona kuwa miongoni mwao walifanikiwa kuchaguliwa kuingia katika vikao vyote viwili vikuu vya maamuzi vya Chama.
Kwa upande mwengine, Liberators hawakufurahi. Liberators hao walishaweka shinikizo kwa Mzee Aboud Jumbe (ambaye ndiye chanzo cha kuingiza damu mpya katika CCM ya wakati huo) kuwa vijana aliowaingiza watakujamgeukia
Hivyo basi, mara baada ya kikao cha Mkutano Mkuu wa Taifa kumalizika mwezi Novemba, 1982, Mzee Aboud Jumbe aliwataka Wajumbe wote wa NEC kutoka Unguja akutane nao Unguja, na Wajumbe wote wa NEC kutoka Pemba akutane nao Pemba. Katika mikutano hiyo, hotuba ya mwalimu wangu, Mzee Aboud Jumbe, ilitushtua wengi. Mzee Aboud Jumbe alishtumu kuwa kuna watu wanaoleta uchochezi kutaka kuvigawa visiwa vya Unguja na Pemba; kutaka kuigawa mikoa, yaani mkoa mmoja dhidi ya mwengine katika kila kisiwa; kutaka kuzigawa wilaya, yaani wilaya moja dhidi ya nyengine katika kila mkoa; na kutaka kuvigawa vijiji, yaani kijiji kimoja dhidi ya chengine katika kila wilaya. Akamalizia kwa kusema kuwa watu hao watahukumiwa na kuonja kile alichokiita “Revolutionary Justice”
Hili lilitushtua wengi, hasa sisi vijana wa wakati huo. Tukakumbuka historia ya Zanzibar tangu Mapinduzi ambapo watu walioshukiwa kuwa wapinzani wa serikali, na hasa wasomi, walivyoshughuli
Hivyo baadhi yetu tuliokuwa Wajumbe wa Sekretariati ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama, hasa sisi kutoka Zanzibar, tukamfuata Mzee Rashid Kawawa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM na Mwenyekiti wa Sekretarieti na kumueleza khofu yetu hiyo. Mzee Kawawa akatuelewa na akaamua iletwe agenda juu ya suala hilo katika kikao
kilichofuata katika Sekretarieti. Agenda ikaletwa.
Ikajadiliwa kwa mapana yake, kisha ikawasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu. Kamati Kuu ikaamua kuunda timu mbili kwenda kuchunguza madai yale
Mwandishi : YAHYA ABDULLAH KHAMIS (MAKAMO)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni